MKUU wa Mkoa wa Ruvuma amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ifikapo Agosti 23,2022 kujitokeza kuhesabiwa Sensa ya Watu na Makazi.
Hayo amesema katika Kijiji cha Najima Wilayani Tunduru wakati akizungumza na wanchi wa Kata ya Najima.
Thomas katika ziara yake ya kwanza katika Wilaya hiyo kuanzia kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amsema zoezi la Sensa la watu na Makzi ni zoezi Nyeti la mpango wa Maendeleo katika Nchi na Mkoa kwa ujumla.
“Kila jambo ni Sensa ili swala ya Aljuma itimie inahitaji watu wazima 40 hiyo ni Sensa na Hata katika Biblia Yusuph na Maria walienda Betherehemu kuhesabiwa baada ya Herode kutanga kila mtu akahesabiwe kwao”.
Amesema Wilaya ya Tunduru kwa Mkoa wa Ruvuma inaukubwa wa kilomita za mraba 18,776 ni ya pili kwa ukubwa baada ya Namtumbo hivyo kama wananchi watajitokeza kuhesabiwa itasaidia kupanga mipango ya maendeleo kwa usahihi.
Mkuu wa Mkoa amesema Sensa iliyopita Wilaya ya Tunduru haikufanya vizuri imesababisha upungufu wa Walimu mashuleni,Barabara kutotengenezwa hayo yamepelekea kuto pata idadi kamili ya watu.
Amesema zoezi hilo la Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kisheria namba 351 inatoa taratibu za kuhesabiwa na nisiri baina yako na karani atakayepita kuhesabu.
“Tunashida ya watoto wenye mahitaji maalumu tusiwafiche majumbani tuwatoe wahesabiwe kwaajili ya maendeleo yetu “.
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi Mkoa wa Ruvuma Mwantumu Athuman amesema ifikapo Agosti 23,2022 wahakikishe wanaacha taarifa za msingi ikiwa majina matatu,watu wote waliolala kuamkia siku ya sense,umri kamili taarifa ya ulemavu, hali ya uchumi pamoja na vitamburisho vya Nida,kitamburisho cha Kupigia kura na Ujasiliamari.
Hata hivyo amesema kwa ambao dini zinaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja ahakikishe anahesabiwa kwenye nyumba moja na kila mtu ahesabiwe mara moja ili kupata taarifa sahihi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 18,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.