MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameweka jiwe la msingi katika Kituo cha afya Matili.
Kituo hicho kipo Kata ya Matili Wilaya ya Mbinga Vijijini kime fikia hatua ya lipu na mpaka kukamilika kitagharimu kiasi cha Shilingi milioni 500.
Mkuu wa Mkoa akizungumza katika ziara hiyo amesema Wilaya ya Mbinga vijijini ni sehemu ya kujifunza katika utekelezaji wa miradi pamoja na ukusanyaji wa mapato ya ndani.
“Hatuwezi kwenda kujifunza sehemu nyingine kwenye maendeleo Mbinga vijijini imeweza kukusanya bilioni 400 na kujenga vituo vya afya kama hivi”.
Thomas ametoa rai kwa Halmashauri zingine kuiga mfano wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ili viweze kujenga vituo vya afya kila mwaka pamoja na madarasa.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amehamasisha wananchi wa Wilaya ya Mbinga kujitokeza kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi ifikapo Agosti 23,2022 kwa mpango wa maendeleo ya miaka 10.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mbinga vijijini George Mhina amesema lengo la ujenzi wa kituo ni kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa Kata ya Matili itakahudumia zaidi ya wakazi 13,000.
Mhina amesema uJenzi ulianza Februari 16,2022 na kutarajia kukamilika Septemba 25,2022 kituo cha Afya kinatarajia kuleta ukombozi kwa wananchi wa Kata hiyo ambayo itasaidia mpaka Kata za jirani.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 19,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.