MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amezindua mradi wa Tathimini ya Afya ya Udongo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa unazalisha mazao mbalimbali kwa wingi na kuongoza kitaifa kwa uzalishaji wa Chakula kwa miaka mitatu mfululizo.
Ibuge amezitaja changamoto ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma tija ya uzalishaji wa mazao ikiwemo tatizo la afya ya udongo katika baadhi ya maeneo.
Hata hivyo Ibuge amesema kutokana na tatizo hilo Mkulima anaweza kuzingatia kanuni zingine zote za kilimo bora bila kupima udongo na uzalishaji wa mazao kuwa chini ya kiwango.
“Uzinduzi wa mradi wa tathimini ya afya ya udongo Mkoa wetu unaenda kutatua changamoto kwa kuwaelimisha wakulima kupima udongo na kuboresha udongo itakayowezesha tija ya uzalishaji”.
Ibuge amesema Kampuni ya OCP imepewa jukumu la kupima udongo nchi nzima na Mkoa wa Ruvuma itapima vijiji 100 ili kuimarisha mkakati wa upimaji wa udongo katika Mkoa wa Ruvuma.
Mtafiti wa Udongo kutoka TARI-Uyole Fredrick Mlowe amsema baada ya kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa udongo hauna afya umefikia kwenye alama nyekundu ambayo inasababisha uzalishaji ambao hauna tija.
Mlowe amesema kupitia uzinduzi huo wa mradi wa tathimini ya upimaji wa afya ya udongo tatizo hilo linaenda kuisha ikiwa mmea unahitaji virutubisho 13 ambavyo vinasababisha lishe katika mmea, kutokana na utafiti umeonyesha udongo wa Ruvuma umekosa virutubisho 10.
“Sisi kama Serikali tumetoa mapendekezo kwa kila mampuni yote yanayozalisha mbolea nchini wafanye jitihada za kutengeneza Mbolea zinazoendana na ukosefu wa virutubisho vilivyokosekana katika udongo”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Mai 12,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.