Utafiti umebaini kuwa robo tatu ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ni hifadhi ikiwemo eneo la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.
Katika shoroba unayounganisha Selous na Niassa nchini Msumbiji kuna hifadhi tatu ndani ya Wilaya ya Namtumbo ambazo ni Mbarang’andu, Kisungule na Kimbanda.
Wilaya ya Namtumbo inahusika katika mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji unaoendelea kutekelezwa na serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mto Luegu unaonzia Wilaya ya Namtumbo unachangia asilimia 19 ya maji katika Mto Rufiji.
Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Mbarang'andu imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka nchi za Ulaya na Marekani ambao wanatembelea jumuiya hiyo yenye vijiji saba na kufanya aina ya utalii ambayo inahusisha moja kwa moja matumizi ya wanyamapori.
Jumuiya hiyo inahusisha vijiji saba ambavyo ni Mchomolo, Kitanda, Likuyuseka Maganga, Kilmasela, Nambecha, Songambele na Mtelemwahi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.