BUSTANI ya asili ya wanyamapori ya Ruhila iliyopo Manispaa ya Songea imeongoza kwa kupokea idadi ya watalii waliofikia 5.461 kati ya watalii 10,069 walifika mkoani Ruvuma katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu.
Akitoa taarifa kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Utalii Mkoa wa Ruvuma ndani ya ukumbi wa Manispaa ya Songea ,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alivitaja vivutio vingine vilivyotembelewa katika kipindi hicho kuwa ni Hifadhi ya Taifa ya mazingira Asilia ya Mwambesi Tunduru ilipokea wageni 637,Makumbusho ya Taifa ya Majimaji wageni 2,977,Makumbusho ya Dkt.Rashidi Kawawa wageni 642 na Hifadhi ya Mazingira ya Matogoro wageni 310.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.