Na Elizabeth Newa - Rs Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 11 mwaka huu kila mmoja ana wajibu wa kufanya kuhakikisha maandalizi yanakamilika kabla ya siku ya uchaguzi.
Kanali Ahmed ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
"Tukio ama shughuli mojawapo ni utoaji wa elimu au kuwapasha habari wananchi kuhusiana na zoezi hili na wajibu wao, hata kikao hiki ni sehemu muhimu ya maandalizi ya uchaguzi huu," alisema Kanali Ahmed.
Ameongeza kuwa tukio lingine ambalo litafanyika kabla ya uchaguzi ni uandikishaji wa wapiga kura ambao utaanza tarehe 11-20 Oktoba, 2024 hivyo amezitaka Wilaya zote na Halmashauri kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.
"Sisi kama wadau ni muhimu tushirikiane kuhakikisha eneo hili linafanikiwa, kama tukifanya vizuri katika maeneo haya matukio mengine ya kampeni na siku ya kupiga kura yatafanyika vizuri,"alisema.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo amesema wote kama wadau wanapaswa kushirikiana kuwahimiza wananchi wajitokeze kujiandikisha ili wapate sifa za kupiga kura.
Kwa upande wake Mratibu wa uchaguzi wa Mkoa wa Ruvuma Salum Kateula amesema lengo la kikao hicho ni kupitia maeneo muhimu yanayohusu kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024.
Ameongeza kuwa wananchi wanaendelea kuelimishwa kuhusu uchaguzi kwa kutumia mabango, matangazo, matamasha, na vikao mbalimbali katika ngazi za Wilaya, kata, na vijiji ambapo Elimu hiyo inalenga kuwawezesha kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kuelewa mchakato mzima hadi siku ya uchaguzi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara ya mwisho ulifanyika tarehe 24 Novemba, 2019 ambapo mwaka huu uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba.
Baadhi ya wadau wa uchaguzi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.