TAMASHA la Mziki Mnene linalo hamasisha utoaji wa Chanjo ya UVIKO 19 kwa jamii limezinduliwa rasmi Ruvuma.
Tamamsha hilo limezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Laban Thomas limefanyika katika Uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea.
Mgema katika uzinduzi huo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alijitokeza hadharani kuchanja Chanjo ya UVIKO 19 Julai 28,2021 ili kuonyesha njia ya kujikinga na Ugonjwa wa Korona.
Amesema Mkoa wa Ruvuma ulizindua Chanjo ya UVIKO 19 Agosti 4,2021 akiongoza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuendelea katika Halmashauri.
Hata hivyo amesema Serikali iliona vyema kuwa na Mpango wa jamii Shirikishi na harakishi ya utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO 19 kama ilivyoelekezwa na utekelezaji ulianza rasmi Septemba 22,2021.
Mgema amesema Mkoa ulipokea Wadau wa kuwezesha kuchanja Aprili ,2022 kama vile USAID FHI360 kupitia mradi wa EpiC,Juni ,2022 Mkoa ulipata mdau USAID- AFYA YANGU na kulenga watu wanaoishi na UKIMWI kufikiwa na huduma ya Chanjo.
“Hadi kufikia Julai 31,2022 Mkoa umechanja watu 703,891 kati ya 957,938 ambao wamekalisha Dozi sawa na asilimia 73 na kuwa kinara kufikia lengo la asilimia 70 Kitaifa”.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Louis Chomboko akizungumza katika Tamasha Hilo amesema wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanamwamko Mkubwa wa kuchanja isipokuwa kwa wananchi wachache,jitihada za kutoa elimu zinaendelea ili kuhakikisha kila mwanaruvuma anafikiwa na Elimu ya Chanjo ya UVIKO 19.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 6,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.