MKOA wa Ruvuma unatarajia kuzindua wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama Duniani,Agosti Mosi,2023 katika Kituo cha Afya kata ya Ruvuma kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuanzia saa 2:30 asubuhi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen ndaki amesema Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambayo itaanza Agosti Mosi hadi 7 mwaka huu.
“Lengo la kuhamasisha unyonyeshaji maziwa ya mama ni kulinda na kuendeleza afua ya unyonyeshaji kama njia mojawapo ya kuboresha hali ya lishe kwa watoto’’,alisisitiza Ndaki.
Hata hivyo amesema kwa mwaka huu wiki ya unyonyeshaji maziwa katika Mkoa wa Ruvuma,itafanyika katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma ambapo ametoa rai kwa viongozi,watendaji na wananchi kushiriki kikamilifu kwenye maadhimisho hayo .
Kaulimbiu ya mwaka huu ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama inasema “Saidia unyonyeshaji,wezesha wazazi kulea Watoto na kufanya kazi zao kila siku’’.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.