Mkoa wa Ruvuma katika Msimu wa kilimo 2023/2024 kuanzia mwezi Julai 2023 hadi kufikia Mwezi Juni, 2024 zimeingizwa jumla ya tani 113,000 na kusambazwa kwa wakulima mahitaji yalikuwa ni tani 112,692. Tani 16,854 zimeendelea kutumika kwenye mazao yasiyotegemea msimu wa mvua na maandalizi ya msimu wa mwaka 2024/25.
Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Onesmo Ngao amesema bei za sokoni za mbolea ni kati ya sh.60,000.00 hadi sh.132,000.00 na bei za ruzuku za mbolea ni kati ya sh.50,000.00 hadi sh.70,000.00 Tunaipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka ruzuku kwenye mbolea ambayo imempunguzia mzigo wa gharama za uzalishaji mkulima.
Amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ilizindua rasmi mfumo wa mbolea za Ruzuku Agosti, 2022 ambapo zoezi la usajili kwa wakulima lilianza tarehe 01 Agosti, 2022. Kwa msimu wa mwaka 2023/2024 na kwamba Mkoa wa Ruvuma umesajili jumla ya wakulima 389,446 kati ya lengo la kusajili wakulima 428,288.00 sawa na asilimia 90.9.
Kwa msimu wa mwaka 2023/24 ya vituo 205 vilisajiliwa na Taasisi ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa ajili ya kutumika kuuza mbolea ya ruzuku kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.