Viongozi wa Taasisi za dini mkoani Ruvuma wahimizwa kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa kuhifadhi mazingira ili kupunguza athari za mabaliko ya tabia ya nchi.
Wito huo umetolewa na Afisa maliasili Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe wakati wa uzinduzi wa progamu ya uhifadhi misitu na mazingira iliyoandaliwa na shirika la utunzaji wa mazingira duniani (WWF)
Challe amesema kuwa Viongozi wa dini wanao wajibu wa kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kupitia mafundisho ya dini kwa kutumia sera mazingira ya mwaka 2022 ili malengo yaliyowekwa na Serikali katika sekta ya uhifadhi mazingira yanatimia.
“Viongozi wadini ni watu ambao wanasikilizwa sana na waumini zao kwahiyo kupitia wao tumeona tuwaharike kama wadau kwa lengo la kuwahimiza na kuwasisitiza juu ya uhifadhi wa upandaji miti ili kuboresha mazingira kwasababu wanamchango mkubwa kwa jamii ”alisema Challe.
Pia amesema katika kusisitiza utunzaji wa mazingira katika mkoa wa Ruvuma kila ifikapo mwezi januari ufanya kampeni ya upandaji miti mkoa mzima kwa kutoa miche laki tatu ambayo utolewa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake mratibu wa progamu za mazingira, utunzaji wa misitu na upandaji miti mkoa wa Ruvuma Ndugu Furuko Hyera amesema progamu hiyo inalenga kutunza aridhi na kupunguza athari za mabaliko ya tabia nchi.
Amesema kupitia programu hiyo itasahidia kufundisha jamii kuhusu kurithisha kwa vizazi kuhusu utunzaji mazingira kwa kupanda miti kuliko kurithisha uvunaji miti holela ambao umekuwa ukisababisha majanga kama vile ukame, mafuriko ambapo athari za majanga hayo hayachagui dini bali yanakuja kwa wote.
“Programu hii itaenda kufundisha jamii kuwa itambue kuwa pale inapotaka au kuvuna miti itambue kwamba wanapovuna miti watambue kunawalioipanda na kuiotesha hivyo jamii inatakiwa kuwa na mazoea kufundisha watoto kupanda miti ili kizazi kijacho kiweze kunifaika na utunzaji mazingira na upandaji miti wa sasa”amesema Hyera
Naye Shekhe wa Mkoa wa Ruvuma Ramadhani Mwakilima amesema anaishukuru shirika la utunzaji wa mazingira duniani (WWF) kwa kutambua mchango wa viongozi wa dini katika kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa misitu
“Sisi kama viongozi wa dini tumelipokea na tumejipanga kuzungumza na kuwahasmisha waumini wetu pia kama taasisi za dini hatuwezi kujitenga na umuhumu wa kuhifadhi na kutunza mazingira” amesema Mkilima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.