Wananchi wa kijiji cha Ndelenyuma katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma,wameiomba serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) kukamilisha kwa wakati mradi huo ili uweze uanze kuwahudumia wananchi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Stanley Ngailo,ameipongeza serikali kwa kutoa fedha zilizoanza kutekeleza mradi wa maji ya bomba.
“kijiji hiki kina changamoto kubwa ya maji safi na salama,hivyo wananchi wanalazimika kununua ndoo moja ya lita 20 kwa bei ya Sh.1,000 gharama ambayo ni kubwa mno,tunaiomba serikai yetu tukufu iharakishe ujenzi wa mradi huu”alisema Ngailo.
Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya Demotoclasa Real Hope ya Dar es slaam Novatus Mwaipopo, ameahidi kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilayani Songea Triphon Mwanangwa amesema mradi huo unaojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 na kwamba ,mradi huo utawanufaisha zaidi ya wakazi 4,331.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.