• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RUWASA Ruvuma ilivyodhamiria kusambaza huduma ya maji vijijini

Imewekwa kuanzia tarehe: February 21st, 2021

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA)  ilianzishwa kwa Sheria namba tano ya huduma ya maji na usafi wa mazingira ya mwaka 2019 na kuanza kutumika rasmi Julai Mosi,2019

Mhandisi Rebman Ganshonga ni Meneja wa RUWASA  Mkoa wa Ruvuma,anabainisha utekelezaji wa miradi ya maji na mwelekeo wa RUWASA mkoani Ruvuma katika utoaji huduma ya maji vijijini.

Mhandisi Ganshonga anataja hali ya upatikanaji huduma ya maji kwa kila Halmashauri hadi kufikia Juni 2019,ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Songea yenye watu 141,427,idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 86,270 sawa na asilimia 61.0 na kwamba Halmashauri hiyo ina vituo vinavyotoa maji 951 kati ya hivyo vinavyofanyakazi ni vituo 590.

Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea RUWASA inahudumia wakazi 90,730,watu wanaopata huduma ya maji ni 45,479 sawa na asilimia 50.0 ambapo idadi ya vituo vya kutolea maji ni 401 kati ya hivyo vituo vinavyofanya kazi ni 372.

“Katika Halmashauri ya Mbinga yenye idadi ya watu 235,648,idadi ya watu wanaopata maji ni 123,648 sawa na asilimia 52.4,idadi ya vituo vya kuchotea maji ni 375,vituo vinavyofanya kazi ni 196’’,anasema Mhandisi Ganshonga.

Kulingana na Meneja huyo,katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo yenye wakazi  226,945,idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 147,515 sawa na asilimia 65.0 na kwamba kuna vituo 939 vya kuchotea maji,kati ya hivyo vituo vinavyofanyakazi ni 484.

Anabainisha zaidi kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru yenye wakazi 256,510,watu wanaopata huduma ya maji ni 164,166 sawa na asilimia 64.0 na kwamba katika Halmashauri hiyo vimejengwa vituo vya kuchotea maji 954 kati ya hivyo vinavyofanyakazi ni 714.

Kwa mujibu wa Meneja RUWASA Mkoa,katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa yenye wakazi146,160,watu wanaopata huduma ya maji ni 73,080 sawa na asilimia 50.0 na kwamba vituo vya kuchotea maji ni 645 kati ya hivyo vinavyofanya kazi ni 312.

Katika Halmashauri ya Madaba yenye wakazi 53,883,idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 33,407 sawa na asilimia 62.0 na kwamba Halmashauri hiyo ina vituo vya kuchotea maji 419,kati ya hivyo vituo vinavyotoa maji ni 267.

Kulingana na Mhandisi Ganshonga,katika Halmashauri ya Mbinga Mji yenye wakazi 68,338,idadi ya watu wanaopata maji ni 32,500 sawa na asilimia 47.7 na kwamba katika Halmashauri hiyo kuna vituo 305 vya kuchotea maji kati ya  hivyo ni vituo vinavyofanyakazi ni 130.

“Kwa ujumla katika Mkoa wa Ruvuma RUWASA inahudumia wakazi 1,219,642,kati yao idadi ya watu wanaopata maji ni 704,065 sawa na asilimia 57.9,jumla ya vituo vya kuchotea maji ni 4,989,vituo vinavyofanyakazi ni 3065’’,anasisitiza Mhandisi Ganshonga.

Hata hivyo anaitaja hali ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma hadi kufikia Desemba 2020 iliwezesha wakazi 833,361 kati ya 1,344,397 kupata maji  sawa na asilimia 62.6.

Anaitaja bajeti ya RUWASA mkoani Ruvuma katika kipindi cha  mwaka wa fedha 2020/2021 imelenga kutekeleza idadi ya miradi ya maji 77  katika Wilaya za Songea,Mbinga,Namtumbo,Tunduru na Nyasa ambapo jumla ya shilingi bilioni 17,095,079,568.15 zimetengwa.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Februari 20,2021

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.