SEKRETARIETI ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala Ndugu Stephen Ndaki Mei 9,2023 imeanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Sekretarieti imekagua mradi wa ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Tunduru ambapo serikali kuu imetoa shilingi milioni 900 kutekeleza mradi huo ambao unatarajia kukamilika Juni 30 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya ukarabati wa hospitali hiyo Bosco Mwingira amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 200 zinakarabati jengo la upasuaji,milioni 400 zinajenga upya majengo ya wagonjwa wa nje na shilingi milioni 300 zinajenga maabara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.