SEKRETARIETI RUVUMA YAKAGUA MRADI SEKONDARI YA WASICHANA YA MKOA KWA SAA NNE
Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imetumia zaidi ya saa nne kukagua mradi mkubwa wa ujenzi wa sekondari ya wasichana Mkoa wa Ruvuma ambayo imetengewa shilingi bilioni nne.
Sekondari hiyo imesajiriwa jina la sekondari ya wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan iliyojengwa eneo la Migelegele Kata ya Rwinga Wilaya ya Namtumbo
Hata hivyo hadi sasa shilingi bilioni tatu zimetumika kutekeleza mradi huo katika sekondari hiyo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 na ambayo inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi Julai 2023.
Baada ya ukaguzi Sekretarieti imeuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha dosari zote zilizojitokeza zinafanyiwa marekebisho kwa wakati
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa kumi ya kwanza ambayo serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa fedha za kujenga sekondari maalum za wasichana za mikoa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.