BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Lusewa na Lingusanguse wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka MtwaraPachani hadi Tunduru yenye urefu wa kilometa 300 ili waweze kuondokana na adha wanayopata wanapopita katika Barabara hiyo hasa wakati wa masika.
Wamesema,Barabara hiyo itakapojengwa kwa kwa lami,itaharakisha usafiri wanapohitaji kwenda makao makuu ya wilaya Namtumbo mjini au makao makuu ya Mkoa Songea kwa ajili ya kufuata huduma mbalimbali ikiwemo za kiserikali.
Abuu Mlanda amesema,ubovu wa barabara inasababisha baadhi ya wagonjwa kufia njiani kabla hawajafika Hospitali ya wilaya au Hospitali ya rufaa Songea kwa ajili ya kupata huduma zaidi za matibabu.
Kwa upande wake Msimamizi wa Barabara hiyo kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Ruvuma Mhandisi Irene Kapinga,amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Namtumbo na Tunduru kuwa, Barabara ya MtwaraPachani-Nalasi itajengwa kwa kiwango cha lami pindi serikali itakapopata fedha.
Kapinga,ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fedha ili kufanya matengenezo ya barabara hiyo inayounganisha wilaya ya Namtumbo na Tunduru
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.