SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais .Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti katika kuhakikisha inaondoa kabisa changamoto ya kukosekana kwa umeme hapa nchini, kuanzia katika ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya,Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga katika hafla ya uwashaji umeme iliyofanyika katika Zahanati ya Lundumato katika Kata ya Ukata.
Amesema“Serikali ya Awamu ya Sita, imejizatiti katika kuhakikisha tunaondoa changamoto ya umeme hapa Ukata, jimbo lote la Mbinga Vijijini lakini kwa wilaya yote ya Mbinga na mkoa wote wa Ruvuma"
Ameendelea kumefafanua kuwa katika Kata ya Ukata kati ya Vijiji vinne vya Litoho, Liwanga, Ukata na Ulima, Vijiji vitatu vimeshapata umeme na Kijiji kimoja kilichobaki kitapata umeme kabla mwaka 2023 haujaisha.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili Mhandisi Evance Kabingo ameeleza kuwa kiasi cha shilingi Bil. 1.19 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa usambazaji wa umeme katika vijiji vinne vya Ukata, vijiji vitatu vimeshafikiwa na miundombinu ya umeme na kijiji kimoja utekelezaji unaendelea.
Utekelezaji wa usambazaji wa umeme unafanyika kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.