Siku ya Ukimwi Duniani, Imeadhimishwa Kitaifa tarehe 01/12/2024, maadhimisho yamefanyika katika Uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
Hafla hii imeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ambaye amesisitiza azma ya serikali kuhakikisha inatokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) nchini.
Katika hotuba yake, Mhe. Dkt. Mpango, ameonesha dhamira ya dhati ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupambana na maambukizi mapya ya VVU.
Takwimu zinaonesha kwamba vijana, hasa wa kike, wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa. Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, serikali imeweka mkazo mkubwa katika kutoa elimu kwa vijana ili kuwasaidia kujitambua, kuchukua hatua za kujikinga, na kwa wale wanaoishi na VVU, kuhakikisha wanafuata taratibu kwa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi (ARVs).
Mhe. Dkt. Mpango ametoa wito kwa jamii nzima kushirikiana, kuhakikisha kwamba maambukizi mapya yanapungua, kwa kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi, matumizi sahihi ya kinga, na upimaji wa afya mara kwa mara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.