• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKAL,I ilivyodhamiria kuwarejesha faru weusi Kusini

Imewekwa kuanzia tarehe: September 26th, 2023

Na Albano Midelo,Songea

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kuona  idadi ya faru Weusi inaongezeka kwa asilimia tano kila mwaka.

Mratibu wa Faru  kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii  Philibert Ngoti amesema hadi kufikia Aprili 2023,idadi ya faru nchini ilifikia 238 hivyo kuvuka lengo la mpango wa Taifa wa kuongeza faru Weusi ambalo lilikuwa ni faru 205 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2023.

“Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1970 hadi 1980 Tanzania ilikuwa na faru Weusi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa nchini waliofikia 10,000 hivyo Tanzania ilijulikana kama nchi yenye faru wengi barani Afrika’’,alisema Ngoti.

Hata hivyo alisema mwanzoni mwa miaka ya 1980 hadi 1990 idadi ya faru ilipungua na kuwa chini ya 100,kutokana na uwindaji haramu na kwamba upungufu wa faru pia ulitokea katika nchi zote zenye faru barani Afrika.

Amesema kutokana na hali hiyo faru Weusi waliwekwa kwenye kundi la Wanyama walio hatarini kutoweka duniani na kwamba mwaka 1993 serikali  ya Tanzania ilikuja na toleo la kwanza la mpango wa Taifa wa miaka mitano la uhifadhi wa faru Weusi.

Mratibu huyo wa Faru Taifa amesisitiza kuwa ,Wizara ya Maliasili na Utalii  imeendelea kuunda sera na mipango ya usimamizi na uhifadhi wa faru Weusi na kwamba mpango huo unaoanzia mwaka 2019 hadi 2023 hivi  upo katika toleo la nne.

Amebainisha zaidi kuwa Mpango wa Taifa wa Uhifadhi na Usimamizi wa Faru Weusi  wa mwaka 2019 hadi 2023 unahimiza kuja na mazao ya utalii kwa kutumia faru Weusi waliopo.

Kulingana na Mratibu huyo,kuna aina tano za faru duniani  kati ya hizo faru weupe wapo wa  aina tatu ambao wanapatikana katika bara la Asia na aina mbili za faru Weusi wanapatikana katika bara la Afrika.

“Nchini kwetu tuna faru Weusi pekee ambao wamegawanyika katika aina mbili ambazo ni faru Weusi wa mashariki na faru Weusi wa kusini kati,faru mweusi aina ya kusini kati anapatikana kusini mwa Tanzania ukiwemo Mkoa wa Ruvuma’’,alisema Ngoti.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  amewaagiza wadau wa utalii kuhakikisha wanaendelea kuwahifadhi Wanyama  faru ambao wapo katika hatari ya kutoweka kutokana na vitendo vya majangili na watu wote wenye nia ovu dhidi ya Wanyama hao.

Amesisitiza kuboreshwa kwa uhifadhi wa Wanyama hao kutasaidia kuendelea kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwepo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Ametoa rai kwa wadau wa maendeleo wakiwemo WWF,GIZ na PALMS kuona umuhimu wa kuanzishwa bustani ya faru katika wilaya ya Namtumbo kwa kuwa tayari eneo ambalo faru Weusi waliwahi kuishi limeainishwa.

Faru mweusi ni mnyama mwenye pembe mbili ,ana uzito wa kilo kati ya 700 hadi 1,500,urefu mita 3.5,ni mnyama mwenye hasira na huwa hatabiriki.

Ni vema mataifa yote ambayo yamebakiwa na faru kushirikiana kuwahifadhi na kuwalinda wanyama hao adimu ambao wapo katika hatari ya kutoweka katika uso wa Dunia.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.