• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI inavyotekeleza miradi ya maendeleo ya bilioni nane Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: November 30th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo yenye thamani ya shilingi bilioni nane.

Katika ziara aliyoifanya Novemba 29 mwaka huu,Kanali Thomas amekagua mradi wa miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambapo Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipofanya ziara  alitoa maagizo ya kurekebisha milango yote 138 iliyopo katika hospitali hiyo ambapo hadi sasa milango 46 imerekebishwa.

Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Chiriku Chilumba kuhakikisha inapofika Desemba 10 mwaka huu kazi zote za umaliziaji ziwe zimekamilika ikiwemo ya kufunga milango yote  katika hospitali hiyo .

Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ni miongoni mwa Halmashauri zinazotekeleza ujenzi wa hospitali kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amesema katika mwaka 2019/2020 serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi  wa majengo ya maabara,mionzi,wodi ya wanaume,wodi ya wazazi na upasuaji,

Kulingana na Mkurugenzi huyo mwaka 2020/2021,serikali ilileta fedha kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ukamilishaji,ujenzi wa njia za kupita wagonjwa na  ujenzi wa wodi ya Watoto.

Amesema mwaka 2020/2021 serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya jengo la upasuaji wanawake,jengo la bima,nyumba ya maiti na ukamilishaji wa wodi ya Watoto.

Hata hivyo amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi milioni 800 kwa ajili ya uendelezaji wa jengo la upasuaji katika wodi ya wanaume,wanawake na nyumba ya maiti.

Akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amekagua mradi  wa ujenzi wa shule ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma inayojengwa eneo la Migelegele ambapo serikali  kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP) imetoa zaidi ya shilingi bilioni tatu kutekeleza mradi huo.

Majengo yanajengwa katika shule hiyo inayotarajia kuanza kuchukua wanafunzi mwakani ni Pamoja na na jengo la utawala, madarasa vyumba 12,mabweni Matano, maabara tatu,vyoo,nyumba za walimu,ukumbi wa shule na bwalo.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameipongeza Kamati ya ujenzi  wa shule hiyo kwa kusimamia vema mradi huo ambapo amesema kila anapotembelea kukagua mradi kumekuwa na mabadiliko makubwa.

Katika ziara hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo,Mkuu wa Mkoa pia amekagua ujenzi wa daraja la Libango lenye urefu wa meta 30 ambapo serikali  imetoa shilingi milioni 900  kutekeleza mradi huo.

Juma Kilaza mkazi wa Libango amesema  wanaishukuru serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambapo awali walikuwa wanapita kwenye kivuko cha miti na kwamba sasa mazao yanayolimwa kwa wingi katika Kijiji cha Libango yatasafirishwa kwa urahisi Kwenda Namtumbo.

Miradi mingine iliyokaguliwa na Mkuu wa Mkoa  ni ukarabati na ujenzi wa  barabara za vumbi la lami za Namtumbo mjini zenye urefu wa kilometa 30  na ujenzi wa kalaveti vyote vikiwa na   thamani ya shilingi milioni 970.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Novemba 29,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.