Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi wa mazingira Songea, Mhandisi Patrick Kibasa amesema kuwa hali ya utapikanaji wa huduma wa maji safi na salama katika Mkoa wa Ruvuma ni asilimia 69 vijijini na asilimia 67 mijini.
Hayo ameyaeleza katika taarifa yake aliyoisoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, kuwa jumla ya miradi 33 yenye thamani ya shilingi bilioni 51.3 inaendelea kutekelezwa vijijini na itakamilika ifikapo Disemba 2023.
“Miradi hii ikikamilika itaongeza huduma ya upatikaniji wa maji vijijini kufikia asilimia 79 ikiwa ongezeko la asilimia 10 lengo ni kutekeleza miradi ya maji vijijini ili kufukia upatikanaji wa huduma kwa silimia 85 ifikapo mwaka 2025”
Aidha, ameeleza kuwa miradi sita ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 148 inaendelea kutekelezwa mijini na inatarajia kukamilika ifikapo mwaka 2025, miradi hiyo ikikamilika itaongeza upatikanaji wa huduma ya maji mijini kwa asilimia 95.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.