TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAAZIMIO YA KIKAO BAINA YA SERIKALI NA UONGOZI
WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA NCHINI.
Thobias Makoba
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dodoma, Juni 27, 2024: Saa 12:00 jioni.
Mtakumbuka kwamba, kwa takribani siku 4 sasa kumekuwa na majadiliano kwa ngazi mbalimbali kati ya Serikali na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara hapa nchini. Mazungumzo haya yalitokana na madai na hoja takribani 41 ambazo wafanyabiashara waliziwasilisha serikalini ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kutokana na hoja hizo, na baada ya vikao na mawaziri wa sekta husika, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia falsafa ya R 4 za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa ile ya Reconciliation kwa maana ya maridhiano, Leo tarehe 27 June, 2024 amehitimisha mazungumzo hayo hapo Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa, kwa niaba ya Serikali Kwa pamoja na uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini wameafikiana kusimamia maazimio 15 ambayo ndani yake serikali imetoa maagizo yafuatayo kwa taasisi husika,
Kutokana na maazimio haya na maagizo ya Serikali, pande zote mbili zimekubakiana hali ya biashara kote nchini kuendelea kama kawaida ili kuwapa watanzania huduma wanazostahili. Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wote kama ambavyo Mheshimiwa Rais amekuwa akisisitiza katika uongozi wake.
Asanteni!
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.