• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yapeleka maji ya bomba kwa wanakijiji Nyasa

Imewekwa kuanzia tarehe: April 5th, 2021

SERIKALI imewatua ndoo kichwani wananchi wa kijiji cha Chimate wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma baada ya kutekeleza mradi wa maji uliogharimu shilingi milioni 390.

Akisoma taarifa ya mradi huo,Meneja RUWASA Wilaya ya Nyasa  Mhandisi Jeremia Maduhu amesema mradi huo ambao umekamilika kwa zaidi ya asilimia 85  unatekelezwa kupitia force account.

Amesema mradi huo utakapokamilika unatarajia kuhudumia wananchi wa kijiji cha Chimate  wapatao 2798 na kwamba maandalizi ya mradi huo yalianza Juni 2020 ambapo kazi rasmi ya ujenzi wa mradi ilianza Julai Mosi,2020.

“Kazi zilizopangwa kutekeleza kwenye mradi huu ni ujenzi wa chanzo kipya cha maji,ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa meta 75,000,ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 15,ujenzi wa mtandao wa bomba wenye urefu wa kilometa 15’’,alisema Maduhu.

Hata hivyo amesema mradi huo hadi sasa zimetumika  zaidi ya shilingi milioni 356 kutekeleza mradi huu ambao unatarajia kukamilika kwa asilimia 100 Aprili mwaka huu.

Amezitaja kazi zilizokamilika kwa asilimia 100 kuwa ni  ujenzi wa chanzo kipya cha maji,tanki la kuhifadhia maji na ujenzi wa vituo 18 vya kuchotea maji.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo,Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema ni jambo la kufuraisha kwamba ameweka jiwe la msingi kwenye mradi huo wakati vituo 10 kati 18 vinatoa maji ambapo amewataka wananchi hao kutunza mradi huo.

Chilumba amewapongeza RUWASA kwa kusimamia kikamilifu mradi huo kuanzia ujenzi hadi kukamilika hali ambayo sasa itawawezesha wananchi wa Chimate kupata maji safi na salama.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga ametoa rai kwa wananchi wa kijiji cha Chimate kuhakikisha kuwa wanasimamia,kutunza na kukilinda chanzo cha maji ili mradi huo uwe endelevu.

“Wananchi wa Chimate,hiki chanzo tunachotumia kwenye mradi huu ni chanzo cha mtiririko,kwa hiyo tafadhali sana msifanye kazi za kibinadamu juu ya chanzo hiki,mkiharibu hiki chanzo mtambue kuwa tutakuwa tumepoteza fedha za serikali bure,maji yatakauka’’,alisisitiza Ganshonga.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wenzake,Mary Ndembeka mkazi wa Chimate amesema,kabla ya mradi huu,baadhi ya akinamama ndoa zao zilikuwa njia panda,huku wengine wakipigwa mara kwa mara na waume zao kwa kuchelewa kutoka kuchota maji mbali ambapo sasa  amefurahi neema imewafikia kwa kupata maji bombani.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Aprili 5,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.