Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS)imesaini Mikataba saba ya ujenzi wa barabara itakayo tekelezwa kwa miaka minne yenye thamani ya shilingi Trillion 3.7 yenye urefu wa kilometa 2035 kwa kiwango cha lami.
Mikataba hiyo imehusisha Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Mpepo – Londo – Lumecha/ Ruvuma, Arusha – Kibaya – Kongwa Construction Of Handeni – Kiberashi – Kijingu – Njoro – Olboroti Mrijo Chini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida Igawa
Akizungumza kwenye hafla hiyo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ameeleza kuwa Barabara hizo zitajengwa Kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F).
Prof.Mbarawa ameeleza kuwa barabara zitakazojengwa zitapita katika Mikoa13 na kufafanua kuwa Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea yenye urefu wa kilometa 435.8 inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta amesema mradi huo ni wa kwanza kufanyika hapa nchini kutokana na ukubwa wake na kueleza kuwa mchakato wa zabuni za EPC+F ulifanyika kupitia ushindani wa uwazi ulioanza tarehe 27 Juni, 2022 ambapo jumla ya Makandarasi 129 walionesha nia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.