• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatoa magari manne na pikipiki 15 kuimarisha ulinzi ikolojia ya Selous-Niassa

Imewekwa kuanzia tarehe: May 27th, 2023

WIZARA ya maliasili na utalii, imekabidhi magari manne na pikipiki kumi na tano kwa Serikali ya mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya kuboresha ulinzi na uhifadhi  wa maliasili katika mfumo wa Ikolojia wa Selous.

Akikabidhi magari na pikipiki hizo kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas,Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Adrehem Nziku amesema,vitendea kazi hivyo vimetolewa na Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya maendeleo ya Ujerumani (KFW).

Amesema,Tanzania inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Ujerumani katika kuhifadhi maliasili ya nchi yetu kwa maslahi mapana ya Watanzania na Dunia kwa ujumla.

Amesema kuwa,juhudi hizi zinaonekana kwa vitendo kwani takwimu za sasa zinaonyesha kuwa takribani robo ya eneo la Tanzania(kilomita za mraba zipatazo 300,000)limehifadhiwa.

Amesema,vitendea kazi hivyo vilivyonunuliwa  kupitia mradi wa SECAD kama sehemu ya utekelezaji wa mradi kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ulinzi na uhifadhi katika ushoroba wa Selous-Niassa zitakwenda kupunguza uhaba wa vitendea kazi katika katika wilaya ya Namtumbo na Tunduru.

Ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa ufadhili wa fedha kiasi cha Euro milioni 18 zilizotolewa kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa maliasili katika mfumo wa Ikolojia wa Selous kupitia mradi wa SECAD.

Aidha,amewapongeza wadau wa uhifadhi( shirika la FZS na WWF)wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi wa SECAD ambao kwa pamoja wamechangia jumla ya  Euro 146,000,00 katika gharama za kutekeleza mradi.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas,amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa maono yake makubwa na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nyanja mbalimbali kuja kuwekeza katika nchi yetu.

Amesema,bila maono yake ya kufungua njia na kusimamia huwenda tusingepata matokeo ya uwekezaji hasa katika sekta ya utalii kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa ambapo Watanzania na Dunia wanaendelea kushuhudia watalii kutoka mataifa mbalimbali wakifika hapa nchini.

Ameishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya maendeleo ya nchi hiyo(KFW),kutoa  magari na pikipiki na wadau shirika la WWF kwa kazi kubwa inayofanya katika kuhakikisha uhifadhi unaendelea kuwepo na kuimarisha mahusiano kati ya wahifadhi na wananchi.

Kwa mujibu wa Kanal Laban,kumekuwa na tatizo kubwa la wanyama wakali na waharibifu katika wilaya ya Namtumbo na Tunduru ambapo kwa muda wa miaka mitatu zaidi ya wananchi ya 24 wameuawa kwa kukanyagwa na Tembo na wengine 21 kujeruhiwa.

Kanal Laban,ametoa wito kwa wizara ya maliasili na utalii na wadau wengine,kusaidia katika uhifadhi wa wanyamapori na maliasili zetu ili ziendelee kutumika kuongeza pato  na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Mkuu wa mkoa,ameagiza magari na pikipiki hizo  zinatakwenda kutumika  kupunguza matukio ya wanyama wakali na waharibifu na kunusuru maisha ya wananchi katika wilaya hizo mbili na siyo vinginevyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Benki ya maendeleo ya Ujerumani Francis Rusengulla amesema, hadi sasa Bebki hiyo imewekeza zaidi ya Euro 100( Sh.bilioni 25) katika uhifadhi  nchii Tanzania.

Amesema,KFW imejikita sana katika sekta ya bioanuwai,ulinzi wa maliasili na kutoa ruzuku kwa  mahitaji ya dharura ndani na nje ya hifadhi za wanyamapori ambapo wakati wa janga la Corona 2020 Serikali ya Ujerumani kupitia KFW ilitoa jumla ya Sh.bilioni 89 za dharura ili kuimarisha uhifadhi hapa nchini.

Pia wametoa mitambo ya kutengeneza barabara,malori ya kubebea mafuta,maji na vifusi pamoja na kujenga vituo vya doria na nyumba za watumishi na ukumbi wa chakula na vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Likuyusekamaganga.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.