SEKRETARIETI ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imekagua ujenzi wa zahanati tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambapo serikali imetoa shilingi milioni 130 kutekeleza miradi hiyo
Zahanati zilizokaguliwa ni Namiungo Kata ya Namiungo ambayo serikali imetoa shilingi milioni 29 ,zahanati ya Namasalau Kata ya Tuwemacho ambayo serikali imetoa shilingi milioni 50 kutekeleza mradi huo na zahanati ya Malombe kata ya Mlingoti ambapo serikali imetoa shilingi milioni 50 kutekeleza mradi huo.
Sekretarieti imeuagiza uongozi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakikisha miradi yote inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.