SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imetoa fedha kiasi cha Tsh 12,854,209,081 kwa ajili ya kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya 25 na nyumba za watumishi kwenye Halmashauri zote n za Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Serikali ya Dkt.John Magufuli pia imeongeza upatikanaji wa dawa katika Mkoa wa Ruvuma kwa kuongeza fedha kutoka Tsh 883,303,792 mwaka 2015 hadi kufikia Tshs. 4,545,139,214 mwaka 2020 ambapo upatikanaji wa dawa umeongezeka kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 96 mwaka 2020.
"Mkoa wetu unaendelea na mapambano katika kukabiliana na tatizo la Kupunguza maambukizi ya UKIMWI ambapo hadi kufikia mwaka 2020, maambukizi ya UKIMWI yamepungua hadi kufikia asilimia 5.6 kutoka asilimia 7 mwaka 2015'',alisema.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema hali ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 katika mkoa wa Ruvuma vimepungua hadi kufikia 5/1000 ukilinganishwa na vifo 12/1000 mwaka 2015 na kwamba vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja vimepungua kutoka vifo 9/1000 mwaka 2015 hadi vifo 3/1000 mwaka 2020 na kutaja hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika sekta ya afya.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 21,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.