Shule ya Msingi Ndengu iliyopo Kijiji cha Likwela Kata ya Nyoni Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imepokea zaidi ya shilingi milioni 34 kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo kupitia mradi wa School Wash Sanitation and Hygiene (SWASH).
Afisa Elimu, Vifaa na Takwimu Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Ndg. Ambrose Ngonyani amekitaja kiasi hicho cha fedha wakati anazungumza katika kikao cha kutambulisha mradi huo wa ujenzi wa
Amesema kuwa Serikali kupitia mradi wa SWASH imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo ili kuendelea kuboresha na kuimarisha miundombuni ya ujifunzaji na ufundishaji.
Aidha Ngonyani amewataka wajumbe hao kuhamasisha wananchi kwa Kijiji cha Likwela kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mradi huo ili uwe mradi wa mfano kwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa na katika ubora unaohitajika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.