Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu imetoa zaidi ya shilingi milioni 900 kujenga sekondari na shule mpya ya msingi katika Kata ya Matarawe Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.
shule mpya zilizojengwa ni pamoja na sekondari mpya ya Philip Mpango iliyotumia zaidi ya shilingi milioni 560 zilizotolewa kupitia Program ya Uboreshaji wa Elimu ya sekondari SEQUIP na ujenzi wa shule mpya ya msingi katika Kata ya Matarawe inayoitwa Matengo Primary School iliyojengwa na serikali kwa zaidi ya shilingi milioni 331 kupitia program ya BOOST.
Sekondari mpya ya Dkt. Philip Mpango imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hadi sasa wapo wanafunzi 162 na shule mpya ya msingi Matengo ina jumla ya wanafunzi 666
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.