SERIKALI YAMALIZA KERO YA MAJI IFINGA MADABA
SERIKALI ya Awamu ya Sita kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa zaidi ya shilingi milioni 480 kutekeleza mradi wa maji katika kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Uzinduzi wa mradi huo umefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas katika kijiji cha Ifinga ambacho kipo takriban kilometa 200 kutoka mjini Songea.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa kijiji hicho kilikuwa kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za maji,barabara na Mawasiliano ya simu za mkononi ambapo serikali imetatua changamoto zote hizo kwa wananchi.
Hata hivyo amesema serikali kwa kushirikiana na wananchi imeanza mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya ili kumaliza changamoto ya Huduma za afya katika kijiji hicho.
Ifinga ni kijiji pekee ambacho kinaunda Kata ya Matumbi katika Halmashauri ya Madaba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.