MADARASA 17 yaliyojengwa Halmashauri ya Madaba kupitia Mradi wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Jamii Covid 19 yakamilika kwa asilimia 100.
Akisoma taarifa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Joseph Mrimi kwa Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde na kuelezea faida ya kukamilika kwa Madarasa hayo.
Amesema Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 340,000,000 kwaajili ya ujenzi wa Madarasa 17 katika shule 7 za Sekondari.
Mrimi amesema mradi huo umesababisha upatikanaji wa madarasa boro ambayo yatawavutia wanafunzi kuja shule kutokana na miundo mbinu bora,samani bora na kuondoa changamoto ya miundombinu.
‘’Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha ambapo miradi imekamilika chini ya uongozi wake thabiti kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025’’.
Mrimi ameelezea changamoto wakati wa wa utekelezaji wa Mradi huo wa Madarasa kutopatikana kirahisi kwa bidhaa za ujenzi wa viwandani,Mfumuko wa bei za vifaa vya viwanda,kuadimika kwa baadhi ya vifaa vya viwandani kama vile bati na saluji.
Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde ameridhishwa na Mradi wa Madarasa 17 yaliyojengwa kupitia Mpango wa Maendeleo ya Utawi wa Taifa amesea madarasa hayo yamejengwa kwa viwango, yatawasaidia Wanafunzi kupata hamasa ya kujisomea kwa bidii na hatimaye kufikia ndoto zao.
Silinde amewapongeza Viongozi wa Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Mkuu wa Wilaya na Watumishi wote kwa kusimamia Miradi hiyo na kuahidi kuendelea kuleta Miradi Mingine katika Halmashauri hiyo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Desemba 17,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.