Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge amemshukuru Mkaguzi Mkuu wa Nje kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi CPA Deogratias Waijaha kwa maelekezo aliyokuwa anayatoa kwenye ukaguzi hali iliyosababisha Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma kupata Hati Safi.
Madenge ametoa shukurani hizo wakati anazungumza katika kikao maalum cha Baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya hoja na mapendekezo CAG kwa hesabu za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanalı Ahmed Abbas Ahmed kwenye Kikao hicho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.