MENEJA Masoko wa Chama Kikuu Cha Ushirika (SONAMCU) Zamakanaly Komba amesema chama hicho kimepata mafanikio makubwa katika kusimamia uuzaji wa mazao ya ufuta,mbaazi na soya katika misimu yote toka kuanzishwa Kwa mfumo wa stakabadhi ghalani Mkoani Ruvuma.
Komba amesema hayo wakati anazungumza kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwenye kikao cha kuzungumzia mafanikio ya mfumo wa stakabadhi ghalani
Komba ameyataja moja ya mafanikio hayo kuwa ni kuwawezesha wakulima wenyewe kuuelewa mfumo wa stakabadhi ghalani na kunufaika na tija iliyopatikana kupitia kuuza mazao yao Kwa mfumo huo katika msimu wa 2022/2023 na 2023/2024.
Komba ameitaja faida nyingine kuwa ni ya wanunuzi wa mazao hayo kuwalipa wakulima Kwa wakati.
Faida nyingine ameitaja kuwa ni kuongezeka Kwa bei ya mazao ya ufuta, soya na mbaazi Kwa kila msimu wa uuzaji wa mazao hayo.
Pamoja na mafanikio hayo Komba ametaja changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutorosha mazao yao na kwenda kuuza nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Juma Pandu ameiomba SONAMCU Kuharakisha mifuko ya kuwekea mazao ya wakulima ili kuondoa malalamiko ya kuchelewesha mifuko hiyo Kwa wakulima .
Pandu ameshauri SONAMCU kuendelea kutoa elimu Kwa wakulima na wafanyabiashara ili waweze Kujua faida ya mfumo huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.