Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amewataka maafisa Elimu Msingi na Sekondari na maafisa lishe kuhakikisha wanasimamia zoezi la wanafunzi kupata chakula chenye viini lishe ili kuondoa hali ya udumavu.
Hayo yamejili katika kikao cha kamati ya lishe cha robo ya tatu ya mwaka ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, watalaamu pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya tathimini ya hali ya Lishe ngazi ya Halmashauri.
Dkt. Sagamiko ametoa rai kwa maafisa Watendaji kata/mitaa kushirikiana na maafisa lishe katika kuhamasisha na kuwaelimisha wazazi wajibu na umuhimu wa kuchangia chakula kwa wanafunzi shuleni katika kipindi cha masomo yao.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dkt. Amos Mwenda amewataka maafisa lishe kufanya ukaguzi wa viwanda vya usindikaji wa chakula kuhakikisha wanakuwa na mashine za kuchanganyia viini lishe.
Alisema Wazabuni wanapaswa kupewa Elimu juu ya kusambaza chakula chenye virutubisho shuleni ili kujenga afya za wanafunzi na kuondoa tatizo la utapia mlo na udumavu katika jamii Manispaa ya Songea.
Naye Afisa Lishe Manispaa ya Songea Albert Sinkamba amewataka maafisa Elimu Msingi na Sekondari kutoa ushirikiano kwa maafisa watendaji kata/mitaa wakati wa kufanya vikao mbalimbali vya wananchi au wazazi na kutoa miongozo kwa wazazi juu ya mustakabali wa kuchangia chakula shuleni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.