Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA) mkoani Ruvuma imeadhimisha Wiki ya Maji 2025 kwa kupanda miti katika chanzo cha Bonde la Mto Ruhila ili kuhifadhi vyanzo vya maji na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji safi kwa wakazi wa Songea.
Zoezi hili ni sehemu ya juhudi za kulinda mazingira na kupambana na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Kaimu Mkurugenzi wa SOUWASA, Maswe Nyamhangwa, amewataka wananchi kuepuka shughuli za kibinadamu zinazoathiri vyanzo vya maji, akisisitiza kuwa uharibifu wa mazingira unaweza kuathiri upatikanaji wa maji kwa vizazi vijavyo.
Serikali imetenga shilingi bilioni 2.8 kwa fidia ya wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji ili kuimarisha juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa SOUWASA, Mhandisi Japhary Yahaya, amesema Bonde la Ruhila linazalisha asilimia 70 ya maji yanayotumiwa katika Manispaa ya Songea.
Amehimiza wananchi kushiriki katika utunzaji wa miti iliyopandwa na kuepuka shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira kama kilimo holela, ukataji miti ovyo, na uchomaji moto misitu.
Maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka 2025 yalianza Machi 16 na yatafikia kilele Machi 22, yakiwa na kauli mbiu “Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji.”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.