• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SOUWASA yakamlisha mradi wa maji Pambazuko kwa asilimia 100

Imewekwa kuanzia tarehe: May 5th, 2023

WIZARA ya maji kupitia mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea(Souwasa),imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Pambazuko kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Uvico-19.

Akitoa taarifa ya ujenzi kwa kiongoziwa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim, msimamizi wa  ujenzi wa mradi huo Franki Tumbi alitaja fedha zilizotumika kutekeleza mradi huo ni  zaidi ya Sh.milioni 578, zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Alisema,lengo kubwa la serikali kujenga mradi wa maji Pambazuko ni katika kutekeleza mkakati wake wa kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa mitaa miwili ya Pambazuko na Mlete yenye wakazi wapatao 3,990.

Aidha alisema,mradi huo utasaidia kuwapunguzia wananchi wa mitaa hiyo miwili muda wa kufuata huduma ya maji  mbali na  makazi yao na kushiriki  vyema katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa mujibu wa Tumbi,vyanzo vya maji vya mardi huo ni visima viwili vyenye wa kuzalisha lita 518,400 kwa siku na mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo  umefikia asilimia 100.

Alisema,mamlaka inatekeleza kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuzingatia na kufuata sera ya maji ya mwaka 2002 ambayo inahakikisha huduma ya maji inapatikana na kumfikia mwananchi katika umbali usiozidi mita 400 kutoka katika makazi yake.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim,amewapongeza wataalam wa Souwasa kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ambao uliojengwa kwa ubora na unaendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na Serikali.

Amewataka wakazi wa mitaa hiyo ,kuhakikisha wanatunza mradi na miundombinu yake ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kutoa huduma ya maji.

Amewakumbusha juu ya wajibu wa kufanya kazi kwa bidii na kutanguliza uzalendo pale wanapotekeleza miradi ya maji ili kwenda sambamba na adhima ya Serikali ya awamu ya sita ya kumtua mama ndoo kichwani.

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Damas Ndumbaro amewakosoa baadhi ya watu wanaohoji kuhusu suala la serikali kukopa fedha kutoka mashirika mbalimbali Ulimwenguni ambapo ameeleza kuwa,fedha hizo zina manufaa makubwa kwa nchi na watanzania kwa ujumla.

Dkt Ndumbaro ambaye ni Waziri wa Sheria na Katiba alisema,fedha zilizokopwa na serikali ya awamu ya sita zimesaidia sana kutekeleza na kuboresha huduma za kijamii hapa nchini ikiwemo ujenzi wa mradi wa maji Pambazuko.

Amewaomba Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao,kumuunga mkono Rais Dkt Samia katika jitihada zake za kuleta maendeleo na kuinua hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.

Mkazi wa mtaa wa Pambazuko Said Kajanja,ameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao umewasaidia kuondokana na changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama.

Alisema,kabla ya mradi huo walikuwa wanatumia maji ya visima vya asili na mito ambayo wakati wa masika hayakuwa safi na salama kwa kuwa yalichanganyika na uchafu mwingi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.