Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira SOUWASA, Mhandisi Patrick Kibasa ametangaza mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mamlaka hiyo imetekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.70, ikiongeza upatikanaji wa maji safi katika Manispaa ya Songea.
Ameitaja miradi mingine inaendelea kutekelezwa, ikiwemo Mradi wa Miji 28 unaotekelezwa katika Manispaa ya Songea wenye thamani ya takriban shilingi bilioni 145.7,
Amesema SOUWASA pia inatekeleza miradi miwili katika kata za pembezoni mwa Manispaa ya Songea. Mradi mmoja unatekelezwa katika Kata ya Subira kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6, na mwingine katika Kata ya Lilambo na sehemu ya Kata ya Lizaboni kwa gharama ya shilingi bilioni 1.5.
Serikali ya Awamu ya Sita pia imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2 kulipa fidia kwa wananchi 975 waliopisha mradi wa maji katika Bonde la Ruhila, ambao walikuwa wakidai fidia tangu mwaka 2003.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.