Ushirika wa Wajasirimali wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO) kwa ushirikiana na Shirika la AGRA Tanzania wamejitambulisha katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo.
Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Revocatus Kimario amesema ushirika huo unatekeleza mradi wa Youth Enterpreneurship for the Future of Food and Agriculture (YEFFA-AJIRA YANGU PROJECT) wenye lengo la kuimarisha ushirikishwaji na uwekezaji wa vijana kuzalisha ajira katika sekta ya kilimo na biashara.
Kimario amesema mradi huo ni wa miezi 36 kuanzia Septemba 2024 hadi Septemba 2027 na unafadhiliwa na Master Card Foundation.
Ameyataja matarajio ya mradi huo kuwa ni kuweza kupata kanzidata yenye taarifa kamili za vijana wanaojihusisha kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo na sekta nyingine ili kuboresha ushirikishwaji na uwezeshaji kupitia program mbalimbali za maendeleo katika sekta ya kilimo hapa nchini.
“Moja ya majukumu muhimu katika kutekeleza mradi huu ni kuhamasisha,kuweka wasifu na kuwezesha vijana 699,496 kujihusha na sekta ya kilimo na biashara katika mikoa saba ya Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe,Ruvuma na Kigoma na kuzalisha fursa za ajira 78,473 za ajira’’,alisema Kimario.
Hata hivyo amesema katika Mkoa wa Ruvuma mradi huo unatarajia kutekelezwa katika Halmashauri za Wilaya ya Songea,Mji Mbinga,Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Namtumbo, Tunduru,Nyasa na Madaba.
Amesema SUGECO inatarajia kushirikiana na wadau wa kimkakati ambao ni serikali,mashirika ya vijana,vyama vya ushirika vya mazao,vikundi vya wakulima,Taasisi za kifedha,Asasi za Kirai na washirika wa AGRA waliopo katika maeneo ya mradi.
Amesema kupitia mradi huo vijana hao watawezesha katika mnyororo wa thamani ya biashara na kilimo iliyochaguliwa kwa kilimo cha alizeti,mazao ya bustani, mahindi, mpunga,maharage na soya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.