MWENGE WA UHURU WATOA TENA KONGOLE KWA RUWASA SONGEA
KIONGOZI wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalah Shaib Kaim ameridhia kuweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Mbangamawe katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ambapo serikali kupitia RUWASA imetoa zaidi ya shilingi milioni 545 kutekeleza mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia wakazi 2,800.
“Nitumie fursa hii kuwapongeza Ndugu zetu wa RUWASA hakika mnafanya kazi kubwa ,mradi ni mzuri una viwango vinavyolingana na thamani ya fedha “,alisema Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Mwenge wa Uhuru Kitaifa ukiwa katika Wilaya ya Tunduru pia uliipongeza RUWASA kwa mradi wa maji wa Muhuwesi uliogharimu shilingi milioni 175,pia RUWASA walipongezwa na Mwenge wa Uhuru katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Ngumbo wilayani Nyasa ambao unagharimu shilingi biulioni 2.5
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.