Taasisi ya Kuzuia na Kapambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake katika robo ya Januari hadi Machi 2024,kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 15 yenye dhamani ya shilingi bilioni kumi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU kwa wanahabari kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo Mahenge mjini Songea.
Haule amesema ufuatiliaji huo umefanyika katika miradi ya ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule mpya za msingi na sekondari,ukarabati wa mabweni na chumba cha maabara zilizoko katika halmashauri za wilaya tano,miradi ikiwa na thamani ya shilingi 3,449,954,835.60
Amesema katika kipindi hicho wamefuatilia ujenzi wa nyumba za watumishi ikiwemo nyumba ya Mkurugenzi na Wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mbinga ,ujenzi wa nyumba za waalimu katika Halmashauri ya Namtumbo na Tunduru zenye thamani ya shilingi 838,859,638/=
Ameongeza kuwa TAKUKURU pia wamefuatilia ujenzi wa miundombinu wa miradi ya maji katika Halmashauri Wilaya ya Nyasa na Halmashauri Wilaya ya Tunduru yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6.8
Hata hivyo amesema TAKUKURU iligundua mapungufu katika miradi miwili yenye thamani ya sh. 4,822,986,357.83/=
TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma inatoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za kufichua vitendo vya Rushwa kwa kutoa taarifa sahihi ili wachukuliwe hatua husika hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.