TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha robo Mwaka Octoba hadi Desemba wamejipanga kufuatilia fedha zilizotolewa na kwaajili ya mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema pamoja na utekelezaji wa robo mwaka wamejiwekea vipaumbele ikiwemo kuendelea kufanya ufuatiliaji katika makusanyo ya fedha za ndani za Halmashauri kupitia utaratibu wa POS.
Mwenda amesema katika kipindi cha miezi 3 ya kumaliza mwaka wataongeza kasi katika kufanya chambuzi za mifumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi kama maeneo ya utoaji wa huduma kwa wananchi na katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa katika miradi ya sekta ya Elimu,Ununuzi,Kilimo,Afya,Uchukukuzi pamoja na uendeshaji wa vyama vya Ushirika.
“Mkoa wetu ni moja kati ya mikoa iliyopata fedha zilizotolewa kwaajili ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19”.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma ametoa rai kwa wahusika wote waliopewa dhamana ya mabilioni kwaajili ya utekelezaji wa Miradi iliyoainishwa kufuata miongozo sahihi ya matumizi ya fedha hizo.
Mwenda ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kutoa ushirikiano Mkubwa kwa Viongozi katika utekelezaji wa miradi iliyoainishwa kupitia mpango wa Maendeleo wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.
Hata hivyo Mwenda amesema kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 iliyoanzia Julai-Septemba 2021 TAKUKURU ilifanya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo (PETS) kumi na tatu yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kubaini mapungufu machache.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Novemba 15,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.