TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Ruvuma imefanikiwa katika ufwatiliaji wa miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 4
Akitoa taarifa ya ufwatiliaji wa utendaji kazi wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Aprili hadi June 2023 , kamanda mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda ,amesema katika kipindi chote TAKUKURU iliendelea kutekeleza majukumu yake
Hata hivyo amesema katika ukaguzi wa miradi kumi , miradi mitano imekutwa na mapungufu na hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuondoa mapungufu hayo
"TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma kwa upande wa uchunguzi tumepokea jumla ya malalamiko 28. Kati ya malalamiko hayo ,malalmiko 26 yalihusu rushwa na uchunguzi wake unaendelea na malalamiko 12 hayakuhusu rushwa hivyo walalamikaji walishauriwa kwenda taasisi husika kupata msaada "
Kulingana na Kamanda Mkuu wa TAKUKURU ,amesema kwa upande wa mashtaka katika kipindi hiki walifungua jumla ya kesi 04, Kesi 03 katika mahakama ya wilaya ya Songea na kesi 01 katika Mahakama ya Wilaya ya Namtumbo ,na kesi hiyo bado inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Namtumbo ,lakini kesi 3 ziliunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Songea zimeisha na Jamhuri ilishinda kesi hizo
amesema kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo kuanzia Mwezi Julai hadi Septemba 2023 wamejipanga kuendelea kuelimisha Wanachi juu ya rushwa na Madhara yake katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.