Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ametangaza tamasha la Ruvuma Toyota 2024 litakalofanyika Novemba 22 na 23 mwaka huu ambalo linalenga kuwahamasisha wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa, utalii, uwekezaji na burudani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Huntclub mjini Songea Kanali Ahmed Ameyataja malengo ya tamasha hilo ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuufungua Mkoa katika sekta za utalili na uwekezaji na kuleta burudani.
"Tamasha la Toyota Festival 2024 kama Mkoa tumeliandaa kuhamasisha kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ili wananchi wajitokeze kwa wingi, kuendeleza jitihada za kuufungua Mkoa katika sekta za utalii na uwekezaji na kuleta burudani kwa wanaruvuma na mikoa jirani ambayo watapata fursa ya kushiriki," alisema Kanali Ahmed.
Amesema kuwa tamasha hilo litazinduliwa Novemba 22 kwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo maeneo ya jirani ndani ya Mkoa wa Ruvuma na kuhitimishwa Mbambabay wilayani Nyasa Novemba 23, ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo kuogelea, kuvuta kamba, muziki na ngoma za asili.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema kuwa tamasha hilo litakuwa na manufaa kiuchumi na kijamii kwa Mkoa wa Ruvuma, watanzania na mwananchi mmoja mmoja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wategi Traders Company, Elizabeth Japheth, amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas kwa jitihada zake katika kuandaa Ruvuma Toyota Festival 2024 na ameikaribisha mikoa jirani kushiriki kwa kuwa lengo ni kuvitangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Mkoani Ruvuma.
Tamasha la Toyota 2024 linameandaliwa na Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Wategi Traders Company, ambalo linalenga kuhamasisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kukuza utalii na uwekezaji, na kutoa burudani kwa wakazi wa Ruvuma na mikoa jirani.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.