AFISA Uhusiano wa Huduma kwa Wateja TANESCO Ruvuma, Allan Njiro, amewatahadharisha wananchi wa vitongoji vya Matemanga na Mkurusi vilivyopo katika kata ya Kigonsera Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vijijini mkoani Ruvuma kuwa makini na watu ambao ni matapeli wanaopita kwenye nyumba zao kwa lengo la kuwaingizia umeme na kuwachaji hela nyingi kinyume na taratibu za shirika hilo.
Hayo ameyasema kwenye ziara yake ya kutoa elimu, kusikiliza kero na kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu umeme ambapo amewataka wananchi hao kuchukuwa tahadhari ya watu matapeli ambao wanapita kwenye nyumba zao na kuwatajia gharama za kuwaingizia umeme wakati serikali inagharamia na wananchi wanatakiwa kulipia kiasi cha sh. 27,000 tu na si vinginevyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.