Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Ruvuma limefanikiwa kuongeza transfoma mpya katika mtaa wa Pachanne B, kata ya Mjimwema, Manispaa ya Songea ili kuimarisha usambazaji wa umeme na kuondoa changamoto ya umeme hafifu.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Ruvuma, Allan Njiro, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za shirika hilo kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa kutosha na wa kuaminika kwa matumizi ya kila siku.
Kuboreka kwa huduma ya umeme kunatajwa kuwa msaada mkubwa kwa viwanda na wakazi wa mtaa huo, ambao hapo awali walikabiliwa na usambazaji duni wa umeme kutokana na kuwepo kwa transfoma moja pekee.
Wananchi, wakiongozwa na Saimon Gabriel Ndewele, wameishukuru TANESCO kwa hatua hiyo
Diwani wa Kata ya Mjimwema, Mheshimiwa Silvester Mhagama, amesema mradi huo utaongeza uzalishaji viwandani na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.
Ameipongeza serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha huduma za umeme na miundombinu nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.