HALMASHAURI ya wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma inazalisha zao la Tangawizi na kuingiza zaidi ya shilingi milioni 16 ya ushuru wa mapato sawa na asilimia 3 kila mwaka .
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake Afisa kilimo,Umwagiliaji na Ushirika(W) Joseph Mrimi amesema kila mwaka inazalisha tani 5,117 na kuuza ndani na nje ya Nchi.
“Halmashauri ya Wilaya ya Madaba tumeweka mkakati wa kuongeza thamani ya zao hilo na kuzalisha kwawingi zaidi ya tani 5117”.amesema Mrilimi.
Mrimi amesema Halmashauri imetenga jumla ya Hekari 400 kwaajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali vya kuchakata mazao ya kilimo ikiwemo zao la Tangawizi.
Hata hivyo amesema wamelitangaza zao hilo katika maonesho ya wakulima nanenane Kanda ya Mbeya na Maonesho siku ya Uwekezaji katika Mkoa wa Ruvuma ,kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma.
“Kampuni ya TANZANICE imeahidi kununuaTangawizi toka kwa wakulima wa Madaba ,na matarajio ya Halmashauri siku zijazo kupata msindikaji mkubwa”.
Mrimi akiendelea kulizungumzia zao hilo amesema Halmashauri imejipanga kuwahamasisha wakulima wanaoweza kulima na kusindika zao hilo ambapo kwasasa mkulima mmoja toka Kijiji cha Ifinga ameweza kulima na kusindika zao hilo.
Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika (W) amesema uongozi wa Halmashauri ya Madaba unaendelea kutoa Elimu kwa wakulima wakishirikiana nataasisi ya RUCCODIA,NOJEPACO CO.LTD na TANZANICE juu ya kilimo Bora ilikuongeza uzalishaji zaidi.
Amesema Halmashauri inashirikiana na SAGCOT kutafuta wadau mbalimbali wakununua na kusindika Tangawizi ili zao hilo liendelee kuongeza uchumi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Desemba 4,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.