WAKALA wa barabara(TANROADS)mkoa wa Ruvuma,katika kipindi cha miaka mitatu imefanikiwa kutekeleza na kukamilisha miradi mbalimbali ya barabara ikiwemo ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66 kwa kiwango cha lami iliyogharimu Sh.bilioni 129.361.
Aidha,TANROADS imekamilisha ujenzi wa daraja kubwa la Ruhuhu lenye urefu wa mita 98.01 linalounganisha wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe ambalo limekamilika na linatumika kwa shughuli za usafiri na usafirishaji.
Hayo yamesemwa jana na meneja wa TANROADS mkoani Ruvuma Mhandisi Saleh Juma,wakati akitoa taarifa ya mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Alisema,daraja hilo limejengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa nguzo za daraja na ulitekelezwa na mkandarasi Lukolo Co Ltd na mhandisi mshauri wa mradi ni kampuni ya Crown Tech-Consult.
Saleh alieleza kuwa,awamu ya pili imehusisha ununuzi na ufungaji wa kitanda cha daraja na kazi iliyofanywa na wataalam wa ndani kutoka(TANROADS) kwa kushirikiana na kampuni ya Jembela Ltd kwa gharama ya Sh.bilioni 8.976.
Pia alisema,wanaendelea na ujenzi wa barabara kutoka Amani Makolo-Ruanda ambayo ni sehemu ya mwendelezo wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kitai-Lituhi-Ndumbi kwa kujenga kilomita 35 kwa kiwango cha lami.
Alisema,mradi huo ulianza mwezi Juni 2022 na ulitakiwa kukamilika mwezi Machi 2024,hata hivyo mkandarasi ameomba kuongezewa muda wa kukamilisha kazi ambapo mhandisi mshauri anapitia maombi hayo ili kujiridhisha na kutoa ushauri kwa wakala.
Alisema,mradi huo unatekelezwa na kampuni ya China Railway Seventh Group(CRSG) kwa gharama ya Sh.bilioni 60.481 na ujenzi wake umefikia asilimia 25.
Akizungumzia ujenzi barabara ya Ruanda-Lituhi-Ndumbi kwa kiwango cha lami Saleh alisema,ujenzi wa sehemu hiyo ni mwendelezo wa ujenzi wa wa barabara ya Kitai-Lituhi-Ndumbi ambayo itaanzia katika kijiji cha Ruanda hadi bandari ya Ndumbi urefu wa kilomita 50.
Alieleza kuwa, kazi ya usanifu imekamilika na zabuni ya mradi huo ilitangazwa tangu tarehe 31 Oktoba mwaka 2022 na serikali imeshatoa kibali cha utekelezaji na TANROADS ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa mradi huo
kwa mujibu wa Mhandisi Saleh ni kwamba,uthamini kwa ajili ya fidia wa mali zitakazo athirika na mradi umekamilika ambapo Sh.bilioni 2.9 zitatumika kulipa.
Alieleza kuwa,kwa sasa ofisi ya TANROADS ipo hatua za uwekwaji wazi taarifa hizo kwa waathirika kabla ya kuwasilishwa kwa mthamini mkuu wa serikali ili itiwe saini kwa ajili ya malipo.
Katika hatua nyingine Saleh alisema,serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya Likuyufusi-Mkenda yenye urefu wa kilomita 124 kuelekea mpaka wa Tanzania na Msumbiji ambayo inatumika kusafirisha mazao na wananchi wa vijiji vya Mkenda,Mkayukayu,Mpitimbi na Likuyufusi.
Alisema,ujenzi wa barabara hiyo utafanyika kwa awamu ambapo awamu ya awamu ya kwanza itajengwa kilomita 62 kutoka Likuyu fusi hadi Mkayukayu na awamu ya pili itatoka Mkayukayu hadi Mkenda umbali wa kilomita 60.
Saleh alisema,usanifu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ulishafanyika tangu mwaka 2013,hata hivyo kutokana na muda mrefu kupita usanifu huo ulifanyiwa marejeo na Tanroads Engineering Consulting Unit(TECU) kwa gharama ya Sh.milioni 178 na kazi hiyo imekamilika mwezi Disemba 2022.
Kwa upande wake msimamizi wa kitengo cha matengenezo Roman Mbukwin alisema,katika miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Tanroads mkoa wa Ruvuma imeendelea kupokea fedha za matengenezo ya barabara ambapo kwa mwaka 2021/2022 walipokea jumla ya Sh.bilioni 20.8,mwaka 2022/2023 Sh.bilioni 19.3 na mwaka 2023/2024 wamepokea Sh.bilioni 17.9.
Naye msimamizi wa miradi ya maendeleo wa Tanroads mkoani Ruvuma Andrew Sanga alisema,katika kipindi cha miaka mitatu wameendelea kufanya matengenezo ya barabara na madaraja katikamaeneo mbalimbali mkoani humo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.