WAKALA wa barabara za mijini na vijijini(Tarura),imetenga kiasi cha Sh.milioni 671 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya dharura Barabara ya Mapera,Mikalanga-Ilela iliyoharibika kutokana na mvua za masika.
Meneja wa TARURA wa wilaya ya Mbinga Oscar Mussa amesema,matengenezo ya barabara hiyo yanafanywa na kampuni ya Ovans Contruction Ltd ili iweze kupitia kwa urahisi na wananchi waitumie katika shughuli zao za usafiri na usafirishaji.
Amesema,mradi huo ni matengenezo ya haraka(dharura) ulianza mwezi Machi na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2023 na kazi zinazofanyika ni ujenzi wa madaraja manne yakiwemo mawili yenye ukubwa wa mita 10,moja la 16 na lingine la mita 5.
Alitaja kazi nyingine zinazofanyika,ni kuchonga barabara wastani wa kilomita 16.96,kuweka kifusi na kutengeneza mifereji ya maji urefu wa kilomita mita 3.
Baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo,wameiomba Serikali kuipatia fedha za kutosha Tarura ili iweze kujenga barabara za vijijini kwa kiwango cha lami badala ya kujengwa kwa udongo ili ziweze kupitika majira yote ya mwaka.
Solanus Ndomba mkazi wa kijiji cha Maguu amesema,wakati umefika kwa serikali kupitia wizara ya Tamisemi kuitengea Tarura fedha nyingi ili iweze kuwa na nguvu kubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara zake ambazo kwa muda mrefu zimesahaulika.
Amesema,barabara za vijijini zina mchango mkubwa kiuchumi kwani zinatumika kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda sokoni,hivyo ni muhimu serikali ikaangalia namna ya kutengeneza barabara hizo kwa lami.
Coster Komba mkazi wa kijiji cha Ugano amesema, mbali ya kusafirisha mazao na bidhaa mbalimbali pia barabara hizo zitasaidia sana kuepuka usumbufu kwa wagonjwa wanaohitajika kuwahishwa katika vituo vya Afya na Hospitali kupata matibabu.
Amesema,wakati wa masika barabara hiyo ni changamoto sana kutokana na mvua zinazonyesha, hali inayolazimu kujifunga na hivyo wananchi kukosa mawasiliano kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Ameishukuru serikali kwa uamuzi wa kufanya matengenezo ya barabara hiyo ambayo ni muhimu na mhimili mkubwa wa uchumi kwa wananchi wa Bonde maarufu la Hagati na wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.