• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA Ruvuma inavyozifanyia ukarabati barabara zilizoharibika na mvua

Imewekwa kuanzia tarehe: May 26th, 2023

SERIKALI kupitia Wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA),imeanza ujenzi wa daraja katika mto Masewe linalounganisha kijiji cha Malindindo na Mikalanga katika Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma.

Meneja wa TARURA  wilayani Mbinga Mhandisi Oscar Mussa alisema,serikali imeamua kujenga daraja katika eneo hilo kutokana na kuathirika vibaya na mvua za masika zilizonyesha kuanzia mwezi Disemba 2022 hadi mwezi Machi 2023.

Alisema,daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 16 na linajengwa na kampuni ya kizalendo ya Ovans Construction Ltd kwa gharama ya Sh.milioni 84 sambamba na ukarabati wa barabara ya Mapera-Mikalanga -Ilela yenye urefu wa kilomita 16.96.

Alisema,kutokana na mvua hizo eneo hilo lilionyesha uhitaji wa kujengwa daraja kutokana na kujaa maji na hivyo kukatisha mawasiliano  kwa wananchi wa maeneo hayo na hivyo kuathiri shughuli za usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

Mussa,amewaomba wananchi kuwa  na matumaini kwa kuwa ujenzi wa daraja utakamilika kwa muda wa mwezi mmoja na nusu,kutoa ushirikiano kwa mafundi na kuwa walinzi wa vifaa vya ujenzi wa daraja hilo.

Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya Ovans Construction Ltd Frank Moyo alisema kuwa, amehaidi kazi hiyo itakamilika kwa muda uliopangwa kutokana na kampuni ya Ovans kuwa na uzoefu wa muda mrefu katika ujenzi wa madaraja na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema licha ya muda wa ujenzi kuwa mfupi,lakini daraja hilo litakuwa bora na imara na kuwaomba wananchi kuanza kujiandaa kutumia  daraja hilo kwa shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali.

Baadhi ya wananchi wakiwemo wanafunzi wa shule ya Sekondari Malindindo,wameipongeza serikali kuanza ujenzi wa daraja katika eneo hilo ambalo kipindi cha masika lilikuwa halipitiki kwa urahisi kutokana na kujaa maji.

Rehema Nchimbi alisema,wakati wa masika eneo hilo ni changamoto kubwa kwani linakuwa na maji mengi yanayotoka milimani,jambo linalowaathiri sana  katika masomo yao kwani wanalazimika kubaki nyumbani na hivyo kukosa vipindi darasani.

Diana Ndunguru, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kujenga daraja,hata hivyo ameiomba Tarura kumsimamia mkandarasi kwa karibu aweze kumaliza kazi kwa muda uliopangwa ili waweze kuondokana na adha ya usafiri na usafirishaji wa mazao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.