• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA Ruvuma yafungua barabara na madaraja

Imewekwa kuanzia tarehe: December 4th, 2022

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kujenga madaraja mawili yenye thamani  ya shilingi bilioni 1.3.

Meneja TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema serikali imetoa shilingi milioni 900 kujenga daraja la Libango wilaya ya Namtumbo ambalo linaunganisha vijiji vya Libangu na Mianzini.

Amesema daraja hilo lenye urefu wa meta 30 lipo umbali wa kilometa 12 kutoka Namtumbo mjini na kwamba daraja limejengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitumika milioni 600 na awamu ya pili shilingi milioni 300.

Meneja TARURA Mkoa amesema katika wilaya ya Namtumbo pekee TARURA pia inatekeleza mradi wa  kivuko chenye kalvati mbili kinachojengwa mjini Namtumbo ambacho kinagharimu shilingi milioni 80.

Ameongeza kuwa serikali pia imetoa shilingi milioni 90 za kukarabati barabara yenye urefu wa kilometa 30 mjini Namtumbo na kujenga barabara ya lami  mjini Namtumbo yenye urefu wa kilometa moja na nusu kwa shilingi milioni 800.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Libango na Mianzini wamemshukuru  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi wa daraja hivyo kumaliza kero kubwa ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi hao.

Mohamed Rajabu Mkazi wa Libango amesema kwa miaka mingi walikuwa wanapata adha kubwa ya  usafiri hasa kusafirisha mazao kutoka katika Kijiji cha Libango ambacho kinazalisha mazao mengi ya chakula.

Ashura Zuberi Mkazi wa Libango amesema daraja hili sasa limekuwa mkombozi hasa kwa akinamama wajawazito ambao walikuwa wanapata shida ya kuvuka wanapokwenda kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo.

“Walikuwa wakifika hapa darajani ,mama anashuka pikipiki inabebwa hadi ng’ambo ya pili,kwa daraja hili tumekombolewa tunamshukuru sana mama yetu,Rais wetu Samia Suluhu Hassan’’,alisema.

Naye Hassan Moyo Mkazi wa Kijiji cha Mianzini amesema kabla ya daraja hili wananchi wa vijiji vya Libango na Mianzini walikuwa wanavuka kwenye kivuko cha miti na kwamba mawasiliano yalikuwa hafifu sana kati ya vijiji hivyo na Namtumbo.

TARURA Mkoa  wa Ruvuma pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa daraja lenye urefu wa meta 25 katika Mto Msinjewe  linalounganisha barabara ya vijiji vya Tuwemacho,Nasya na Mtina  wilayani Tunduru.

Mwakilishi wa Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma  ambaye pia ni Meneja TARURA Wilaya ya Tunduru Mhandisi Silivanus Ngonyani amesema  serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 326 kutekeleza mradi wa ujenzi wa daraja hilo ulioanza Aprili 2022 na unatarajia kukamilika  Desemba 2022.

Salehe Ally Mohamed Mkazi wa Kijiji cha Tumewacho wilayani Tunduru amesema wanaishukuru serikali kwa kuwajengea daraja hilo kwa sababu wakati wa masika baadhi ya watu walikuwa wanapoteza Maisha wakati wanavuka ambapo kwa mwaka jana pekee watu wawili wamekufa.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza TARURA kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ambayo inakwenda kumaliza kero ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Namtumbo na Tunduru.

Amesema daraja hilo lenye uwezo wa kuvusha magari yenye uzito wa tani 25 litawezesha kusafirisha mazao ya wakulima  hasa zao la korosho kutoka tarafa za Namasakata,Lukumbule na Nalasi zenye uzalishaji mkubwa wa zao la korosho.

Kanali Thomas amemshukuru Rais kwa kutoa fedha nyingi zinazotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma ikiwemo ujenzi wa madaraja,vivuko na barabara.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Desemba 4,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.