WAKALA wa barabara za vijijini na mijini Tanzania(TARURA)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,imeanza kuzifungua barabara za kimkakati kwenye maeneo yenye shughuli za uzalishaji ili kuharakisha maendeleo katika maeneo hayo na wilaya ya Namtumbo.
Meneja wa Tarura wilayani Namtumbo Mhandisi Fabian Lugalaba amesema, barabara hizo zitawasaidia wakulima kusafirisha mazao yao kutoka shambani hadi sokoni,kupata bei nzuri na kukomesha tabia ya wafanyabiashara wanaokwenda mashambani kununua mazao kwa bei ndogo isiyolingana na gharama za uzalishaji.
Lugalaba alisema,kwa fedha 2022/2023 wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura) imetumia zaidi ya shilingi milioni 40 kufanya matengenezo ya barabara mpya mbili ya Minazini-Muungano na Barabara ya Mtonya-Irrigation yenye urefu wa kilomita 14 ambapo alieleza kuwa,kukamilika kwa barabara hiyo na nyingine zinazoendelea kujengwa wilayani humo ni mafanikio makubwa tangu serikali ya awamu ya pili ilipoingia madarakani.
Lugalaba ameeleza kuwa,sehemu kubwa ya barabara hizo zimepita kwenye maeneo ambayo wananchi wake wamejikita zaidi na kilimo cha umwagiliaji ambacho kina mchango mkubwa wa kiuchumi kutokana na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ikiwemo kahawa,mahindi na mpunga.
Kwa mujibu wa Lugalaba ni kwamba,tangu Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na sasa Tanzania maeneo hayo hayakuwa na barabara kabisa ambapo wakulima walilazimika kusafirisha mazao yao kwa ubeba kichwani,jambo lililowaathiri sana katika jitihada zao za kujikwamua na umaskini.
Alisema,serikali ya awamu ya sita kupitia fedha za tozo imetambua umuhimu na shughuli zinazofanyika katika maeneo hayo,imefanya matengenezo ya kuzifungua barabara hizo ambazo kwa sasa zimekamilika na zimeanza kupitika.
Baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katika maeneo hayo wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassa na serikali yake ya awamu ya sita kwa kutoa fedha zilizotumika kuzifungua barabara hizo ambazo zinakwenda kuchochea maendeleo na uchumi wao.
Babu Ponera alisema,hapo awali wananchi hususani wakulima wa maeneo hayo walipata shida kubwa ya kubeba mbolea kichwani kutoka kijijini kupeleka shambani,jambo ambalo lilisababisha wakulima wengi kutofikia malengo ya uzalishaji.
Ponera,ameipongeza serikali kwa kuifungua barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa wilaya ya Namtumbo kutokana na maeneo hayo kuwa yenye uzalishaji mkubwa wa mazao katika wilaya ya Namtumbo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.